Wednesday, December 5, 2012

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YATOA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA KUBORESHA MFUMO MPYA WA UTOAJI HUDUMA ZA MATIBABU KWA NJIA YA MAWASILIANO (TELE MEDICINE)

Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu kusini Deograsias Moyo kwa niaba ya mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania akimkabidhi hundi ya zaidi ya sh milioni 15 mkurugenzi wa hospitali ya rufaa Mbeya eliuter Samnkey 

ZAIDI  ya shilingi million 15 zimetolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzanzania (TCRA)  nyanda za juu kusini   ajiri ya  kuboresha mfumo  mpya wa utoaji  huduma za matibabu kwa njia ya mawasiliano (TELE MEDICINE) ili kupunguza vifo na  gharama za usafiri kwa wagonjwa.


 Mhandisi  na kaimu meneja wa mamlaka ya mawasiliano ya simu (TTCL) George Mtikila akipokea hundi hiyo  kwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa dr Eliuter Samnkey kwa ajili ya kuleta vifaa hivyo na kufunga katika hospitali hiyo ya rufaa Mbeya

ZAIDI  ya shilingi million 15 zimetolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzanzania (TCRA)  nyanda za juu kusini   ajiri ya  kuboresha mfumo  mpya wa utoaji  huduma za matibabu kwa njia ya mawasiliano (TELE MEDICINE) ili kupunguza vifo na  gharama za usafiri kwa wagonjwa.

Mkurugenzi  Mkuu wa Hosptal ya Rufaa jijini Mbeya Eleuter Samky alishukuru mamlaka hiyo na kueleza kuwa mfumo huo utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa   kupunguza  vifo na jamii kupatiwa huduma bora licha kuwepo na changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa.
“Mfumo huu utatusaidia sana na kuweza kuokoa maisha ya watanzania kwani kutakuwepo na mawasiliano mazuri na kuelimishana njia mbalimbali za kuweza kutoa matibabu kwa wagonjwa wetu hususan magonjwa ya watoto  na mgonjwa sugu yaliyoshindikana kutibika“Alisema.

Mhandisi  na kaimu meneja wa shirika la simu (TTCL) George Mtikila alisema kuwa  mkataba huo  wameingia na mamlaka ya mawasiliano (TCRA) utaanza kutumika kwa wakati na kwamba  lengo kuu ni kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa  katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi.

Jengo la TTCL Mbeya
Mitambo ya kisasa ya mkonge wa taifa
Hudi iliyokabidhiwa leo
Moja ya wataalam wa mkonge wa taifa Humphrey Ngowi akiwaeleza waandishi wa habari jinsi mtambo huo unavyofanya kazi.

 HIVI NI KWELI HUDUMA ZOTE KWA WAJAWAZITO HUTOLEWA BURE? MAANA KUNA BAADHI YA HOSPITALI KUBWA HAPA JIJINI MBEYA MPAKA SASA WAJAWAZITO WANAKUJA NA VIFAA VYAO

 

HII NDIYO HALI HALISI MBEYA YETU IMEIKUTA KATIKA HOSPITALI KUBWA SANA HAPA MKOANI MBEYA KWENYE WODI YA WAMAMA WAJAWAZITO WALIOFANYIWA UPASUAJI HUAMBIWA WAKANUNUE DAWA NA VIFAA VINGINE VYA MATIBABUHUKU UKUTANI KUMEBADIKWA TANGAZO LA KUWA HUDUMA KWA WAJAWAZITO NI BURE PICHA HIYO INAJIELEZA JAMAA KATOKA KUNUNUA DAWA ZA KUMUHUDUMIA MKE WAKE ALIYEFANYIWA UPASUAJI HOSPITALINI HAPO MBEYA YETU INAENDELEA KUFUATILIA MATUKIO HAYO TUTAZIDI KUWAJULISHA.

Shirika lisilo la kiserikali la Jamhuri ya Czech BEZ MAMY limeanza kampeni ya kukusanya pesa Ulaya kwa ajili ya Kusaidia watoto yatima nchini Tanzania hasa mkoani Mbeya

Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia akiwa na wadau wa Czech BEZ MAMY 
Michoro ya picha za tingatinga inayotumika kukusanya michango hiyo
Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia akiendesha moja ya semina za kuchangia mfuko huo

Shirika lisilo la kiserikali la Jamhuri ya Czech BEZ MAMY limeanza kampeni ya kukusanya pesa Ulaya kwa ajili ya Kusaidia watoto yatima nchini Tanzania hasa mkoani Mbeya
Bez Mamy kwa kushirikiana na shirika la Kitanzania la jiji Mbeya Without Mother Organization kwa pamoja wamedhamiria kuinua elimu mkoani Mbeya kwa kusaidia ukarabati na utoaji wa misaada kwa shule za msingi jijini Mbeya, Ujenzi wa vituo vya watoto yatima, kuwalipia ada watoto yatima na kuboresha huduma za Afya jijini na wilaya mbalimbali za mkoa wa Mbeya
Akiongea na blog hii Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia alisema, wanatumia njia mbalimbali kukusanya pesa  hizo ambazo zitatumika katika ujenzi wa Bweni la wasichana katika kituo cha watoto yatima Mahango,Mswiswi pamoja na ujenzi wa Sekondari ya Ufundi katika Kijiji hicho cha Mahango
Njia zinazotumika kukusanya pesa hizo ni uuzaji wa michoro ya Tinga Tinga katika sehemu Mbalimbali nchini Slovakia na Jamhuri ya Czech na pia kupitia mtandao www.tingatingashop.cz
Njia nyingine ni utoaji wa Mihadhari katika vyuo vikuu, shule za sekondari za ufundi, Makanisani na kwa watu binafsi katika nchi hizo
Akizungumzia misaada na miradi hii bwa Chris Zacharia alisema,Ikiwa watu wa Ulaya wanajitoa kusaidia watoto wa afrika itawatia moyo zaidi kusaidia ikiwa watasikia watanzania wengine wenye uwezo pamoja na serikali wanajitoa kusaidia kundeleza miradi hii ambayo ina msaada mkubwa kwa uchumi na maendeleo ya nchi yetu

SOKO LA MWANJELWA MBEYA LAFIKIA ASILIMIA 80 YA UJENZI

SOKO KUU LA MWANJELWA LINALOENDELEA KUJENGWA MPAKA SASA LIMEFIKIA ASILIMIA 80 ILI KUKAMILIKA NA KUANZA KUFANYA KAZI
WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA WANAPATA MAELEKEZO YA HATUA ILIPOFIKIA YA UJENZI NA NINI KILICHOBAKI ILI JENGO LIANZE KUFANYA KAZI
HILI NI JENGO LA KUHIFADHIA TAKA SOKONI HAPO KABLA YA KUPELEKWA DAMPO



JENGO LA SOKO LA MWANJELWA LILIANZA KUJENGWA 25.02.2010  HADI SASA LIMEFIKIA HATUA YA UMALIZIAJI JAPO LIMECHELEWA KUKAMILIKA NA HATUA ZILIZOPO SASA KUFUATANA NA MKATABA WA UJENZI WA SOKO HILO NI KUWA MKANDALASI ANAKATWA TSH MILION KUMI KILA SIKU KWA MIEZI MITATU ALIYOPEWA AMALIZER NA KUKABIDHI JENGO LIKIWA LIMEKAMIRIKA.

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI ILILENGA KUJIONEA UJENZI UNAVYOENDELEA NA KUJUA KWA NINI JENGO LIMECHELEWESHWA KUMARIZIKA NA HATUA GANI ZIMECHUKULIWA ILI KUKAMILISHA JENGO HILO AMBALO LINA UWEZO WA KUWA NA VYUMBA VYA BIASHARA 450, STOR 3 KWA AJILI YA KUTUNZIA VITU, OFISI MBALIMBALI, POLISI POST MOJA, HOTEL 4, MADUKA MAKUBWA  WATAGAWA KWA MITA, MABUCHA 10, SEHEM YA WAFANYA BIASHARA WADOGO 444, SEHEM YA KUPAKI GALI 150, SEHEM YA KUHIFADHIA TAKA, MAJI SAFI, MAJI TAKA, GENERETA KUBWA, VYOO KWA AJILI YA WAHITAJI MAALUM NA VYA KAWAIDA KATIKA KILA GHOROFA. JENGO LITAKUWA NA GHOROFA 3.
HADI HATUA HII YA ASILIMIA 80 JENGO LIMEGHARIM TSH BILION 8.8 NA HADI UKAMINIKA LITAGHARIMU TSH BILION 13.
Picha na taarifa zote kwa hisani ya Mbeya Yetu.