Kwa niaba ya Asasi isiyo ya kiserikali (CHIPRO) ninapenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Vodacom/Vodacom
Foundation kwa kuandaa chakula cha mchana, vifaa vya shule na vyakula
mbalimbali ( Christmas 2011) kwa watoto
yatima na watoto waishio mazingira hatarishi 500, watoto hawa walitoka katika
asasi mbalimbali zilizopo jijini Mbeya.
Watoto na walezi wao walifurahi sana sana!
Watoto na walezi hawa wamekuwa wakiniuliza je mwaka 2012 tutakula, kunywa na kufurahi pamoja kama mwaka 2011?????? Sina jibu la kuwapa mpaka sasa, Ninamwachia Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma atatenda miujiza yake!!!
Hivyo basi endapo utakuwa umeguswa na ombi la watoto hawa tafadhali wasiliana nasi kwa simu 0754301830. Ubarikiwe sana!
 |
Watoto na wageni waalikwa wakiburudika kabla mgeni rasmi hajafika |
Hapo chachaaaaa!!!!! (Ni furaha iliyoje!!! (FURAHA YAKO NINI??????)
 |
Muandaaji wa shughuli bwana Mkama akizungumza na watoto /wageni waalikwa |
 |
Aliyekuwa Meneja wa Vodacom mkoa wa Mbeya bwana Kiswaga akiongea maneno mafupi kumkaribisha mgeni rasmi (aliyekuwa mkuu wa Wilaya bwana E. Balama)
 |
Afisa Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Mbeya |
|
|
 |
Mmoja wa Kiongozi wa asasi akisoma risala kwa mgeni rasmi |
 |
Mgeni rasmi Akiwasalimia na kuzungumza machache, baada ya kupokea risala |
Muda wa maakuli ulifika, wafanyakazi wa Vodacom ndio waliotoa huduma ya chakula kwa watoto
 |
Huduma cha chakula zikiendelea |
 |
Hawa ni watoto yatima, na baadhi wameokotwa baada ya kuachwa na wazazi/mzazi, umri wao ni kuanzia miaka 0-4, ambao wanalelewa na moja ya Asasi zilizoko mkoani Mbeya (Wanahitaji walezi), kama umeguswa unaweza kumchukua mtoto mmoja kwa makubaliano na asasi husika. |
 |
Bwana Poyo akiwa ameongozoana na kiongozi wa asasi mjawapo |
 |
Bwana Mwakifulefule akitoa huduma kwa watoto hao |
 |
Watoto wakiendelea kupata chakula cha mchana |
 |
Bwana Kiswaga akitoa huduma kwa watoto hawa |
 |
Bi Grace Lyon akiwa amembeba kichanga kilichookotwa wiki moja kabla ya tukio |
 |
Bi Zahra M. Mansour, na wadau wengine wakiendelea kutoa huduma kwa watoto |
 |
Mzazi utamjua tu!!! |
 |
Mzazi utamjua tu!!!, watoto wamefurahi!! |
|
|
|
|
|
 |
Bwana Mramba hakuwa nyuma pia kutoa huduma kwa watoto |
 |
Waandaji wa shughuli wakiteta jambo (Bwana Mkama na bi Zahra) |
 |
Bwana Kapinga nae alikuwepo |
 |
Huduma zikiendelea kutolewa |
 |
Walezi na viongozi wa Asasi mbalimbali |
 |
Muda wa zawadi huuooo!!!!!!!!!!!!!!! Watoto na vikundi vilivyohudhuria vilipewa zawadi zao |
 |
Mmoja wa washiriki wa Asasi wakimshukuru dada Grace Lyon kwa niaba ya kampuni ya simu ya VODACOM/ VODACOM FOUNDATION |
 |
Mgeni rasmi akiondoka baada ya kumaliza sherehe | | | |
|
|
Kwa niaba ya baadhi Asasi zisizo za Kiserikali (CHIPRO), mkoa wa Mbeya, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya simu ya VODACOM/VODACOM FOUNDATION, kwa chakula cha mchana , vifaa vya shule, na vyakula mbalimbali, kwa watoto waishio mazingira magumu na yatima katika mkoa wa Mbeya.
Nitakuwa mkosefu wa fadhila endapo sitatoa shukrani zangu za pekee kwa dada Grace Lyon, bwana Yessaya Mwakifulefule, bwana Mkama na wengineo wote waliosaidiana nasi kufanikisha shughuli hii.
Pia napenda kumshukuru bwana E. Balama kwa kukubali kushirikiana nasi! Mwenyezi Mungu awabariki sana!