Tuesday, November 27, 2012

MTOTO ALIYECHOMWA MKONO NA HATIMAE KUKATWA MKONO WAKE WA KUSHOTO ALETWA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI

MTOTO ANETH KATIKATI NA MAMA YAKE KULIA WAKIINGIA ENEO LA MAHAKAMANI LEO

WILVINA MKANDALA ANAETUHUMIWA KWA KUMUUNGUZA NA KUSABABISHA KUKATWA KWA MKONO WA MTOTO ANETH AKIINGIZWA MAHAKAMANI HUKU AKIWA HATAKI KABISA KUPIGWA PICHA
WAKAZI WENGI WA JIJI LA MBEYA NA VITONGOJI VYAKE WAMEJITOKEZA KWA WINGI KUJA SIKILIZA KESI HIYO

MTOTO ANETH AKISALIMIANA NA MAMA ALIYEMUHUDUMIA HOSPITALINI KABLA YA MAMA YAKE MZAZI KUJA TOKA BUKOBA
MAMA ANETH AKIONDOKA NA MWANAE MARA BAADA YA HAKIMU KUMUONA MTOTO HUYO NA KUPATA MAELEZO MAFUPI TOKA KWA MTOTO ANETH AMBAE ALISHINDWA KABISA KUONGEA MARA TU ALIPO MUONA SHANGAZI YAKE HUYO ALIYEMCHOMA MOTO AKIINGIA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA KESI HIYO IMEAIRISHWA MPAKA TAREHE 6/12 / 2012
MTOTO ANETH MARA TU BAADA YA KUTOKA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA AKISUBIRI KURUDISHWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA KUENDELEA NA MATIBABU
HUKU AKINA MAMA WAKIWA NA JAZBA YA KUTAKA HAKIMU AWAACHIE KIDOGO JAPO KWA DAKIKA TANO WAMFUNZE ADABU MTUHUMIWA HUYO KWANI WANADAI AMEWADHALILISHA SANA KWA KITE

Mwanamke anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto wa kaka yake kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.

Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24)
Hataki kabisa kuonyesha sura yake

Aneth akiwa na wazazi wake mahakamani jana
Akirudishwa tena rumande mpaka tena tarehe 27/11

Baadhi ya akina mama wakiwa nje ya mahamaka wakisubiria kumwona mama huyo mwenye roho mbaya
Akina mama hao wakiwa na hasira kali walisikika wakisema tuachieni kidogo tumfunze adabu


MWANAMKE
anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto  mtoto wa kaka  yake  kumfungia ndani,  amepandishwa    kizimbani kwa mara ya pili    katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu
shtaka linalomkabili.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameileza  Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24)
Mkazi wa Majengo jijini humo  alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa
na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto  Aneth Gasto (4).
Mulisa
akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert
Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu  cha
222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
 Kutokana na hali hiyo
mwendasha mashitaka huyo ameileza mahakama kuwa kesi inayo mkabili mwanamke
huyo ilihitaji mashahidi sita   ambao ni Dactari aliye mfanyia upasuaji mtoto
huyo   mwenyekiti wa Mtaa na barozi wake pamoja na Askari
mpelelezi wa kesi hiyo na mtoto mwenye .
 
Amesema
teyari mashahidi wanne kati ya sita wamekwisha toa ushahidi wao mahakani hapo .
Kutokana
na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo alirudishwa mahabusu hadi
Novemba 27 Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Amesema
upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao watatu kati yao teyari wamekwsha toa
ushahidi wao katika mahakama hiyo .
  
Amewataja
mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shuku Mwakanyamale, Daktari
anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul Kasubi  na Habiba Mwakanyamale .
Wengine
ni Askari Polisi aliyepeleza kesi hiyo WP Pudensia na Mtoto mwenyewe  ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa
ushahidi wao mbele ya mahakama.
Awali
mshatakiwqa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto  huyo ambapo
pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo
na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP)
kwenye mkono uliobaki.
Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu

No comments: