Tarehe 07/10/2012 ilikuwa siku ya huzuni sana kwangu na familia
yangu, hasa baada ya kuondokewa na mama yangu mpendwa (Mama Martha)
ambaye nilifanya nae kazi (WRP)
kwa kipindi cha miaka 7. Alikuwa ni mama
ambaye aliniheshimu, kunifariji, kunishauri nk. , alikuwa ni mama ambaye ni mchapa
kazi, na mwenye moyo wa kujifunza na kujitolea ! She was a real model mother!
Kwa
niaba ya familia yangu, ninapenda kutoa pole kwa familia ya bwana
Mwihomeke wa Block T, Mbeya kwa kufiwa na mke (mama Martha Mwihomeke)
Pia napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa madaktari na wafanyakazi wote waliomuuguza hasa hospitali ya Rufaa,Mbeya.
Kwani Mungu alimpenda zaidi.
Mwenyezi Mungu apumzishe roho yake mahali pema peponi:AMINA!
Picha zote kwa hisani ya Joel Jailos,Mbeya
 |
Mume wa marehemu (mzee Mwihomeke) akitoa salamu za shukurani kwa ndugu, jamaa na marafiki |
|
|