Wednesday, November 14, 2012

HATIMAE MTOTO ANETH SASA AENDELEA VIZURI BAADA YA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO JANA

MTOTO ANETH AKIWA ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUMKATA MKONO WAKE WA KUSHOTO JANA
ANETH AKUTAYARISHIWA CHAKULA NA MAMA YAKE MDOGO SLIVIA ANAEMUHUDUMIA HOSPITALINI HAPO
KWA UJUMLA MTOTO ANETH SASA ANAENDELEA VIZURI NA ANAKULA CHAKULA VIZURI PIA TAARIFA TULIZOPATA MUDA SI MREFU MAMA YAKE MZAZI YUPO NJIANI KUJA MBEYA TOKA KAGERA

HALI ya Mtoto Aneth Johanes (4) aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kufuatia kuchomwa moto  mkono wake wa kushoto na anayedaiwa kuwa ni Shangazi  yake inaendelea vizuri licha ya kufanyiwa upasuaji uliolazimu kukatwa kwa mkono huo.
Kwa mujibu wa mama mdogo wa mgonjwa anayemhudumia  hospitalini hapo Silvia  Salvatory  alithibitisha kuendelea vizuri  kwa motto huyo ambapo alisema ilimlazimu kufanyiwa upasuaji kutokana na mkono huo kukosa mawasiliano na kuonekana kuvunjika.
Alisema  taarifa za awali zinaonesha shangazi yake huyo  Bahati Rukangara alianza kumtesa mtoto huyo muda mrefu mara baada ya kumchukua kutoka kwa wazazi wake wanaoishi Bukoba Mkoani Kagera.
Aliongeza kuwa  tangu amchukue  kwa wazazi wake Februari  Mwaka huu amewahi kumjeruhi mkono wake wa Kulia hadi kuuvunja ambapo hadi sasa mtoto huyo alikuwa akitegemea mkono wa kulia ambao nao umekatwa.
Tukio hilo la kisikitisha lilitokea juzi majira ya saa nne asubuhi baada ya majirani kusikia yowe la mtoto huyo akiomba msaada kutokana na mateso na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhabu hiyo kutoka kwa Shangazi yake
.
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Thomas Isidori  alisema hali iliyopelekea kukatwa kwa mkono wa mtoto huyo  ni siri kati yake na daktari aliyemhudumia  na kwamba  sheria ya uuguzi inakataza kutoa taarifa ambazo ni siri.
Isidori alipoulizwa sababu za mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji mapema mno hadi kusababisha ulemavu alisema ni suala la kitaalamu ambalo hata yeye hawezi kulijibu na ni sheria ambayo inawataka madaktari kutunza siri za wagonjwa.
Hata hivyo muuguzi huyo alizuia kabisa waandishi wa habari kupiga picha za motto huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo uliosababisha kukatwa mkono kwa mgonjwa huyo.
Baadhi ya wananchi waliofika Hospitalini hapo kumjulia hali mtoto Aneth aliyelazwa Wodi namba Nane ambao  hawakutaka kutaja majina yao walilaani kitendo cha madaktari kukimbilia kukata mkono mgonjwa badala ya kujaribu njia zingine za kunusuru hali hiyo.
Habari kwa hisani ya Venance Matinya, Picha na Mbeya yetu
 

MTOTO ALIYEUNGUZWA MKONO NA KULISHWA KINYESI AKATWA MKONO HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA


Hatimaye yule mtoto aliyechomwa moto na mama yake amekatwa mkono wake wa kushoto




Bahati Rukangara huyu ndiye aliyemchoma mtoto Janeth

habari kamili tutazidi kuwaletea


picha na kalulunga
             

MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA MC BARAKA CHAWE ISYONJE MBEYA

BAADHI YA WASHEREHESHAJI  WA JIJI LA MBEYA WAKIWA WAMEBEBA MSARABA NA PICHA YA MAREHEBU BARAKA CHAWE WAKIELEKEA ENEO LA IBADA YA MWISHO YA KUMWOMBEA MAREHEMU CHAWE
MA MC WAJIJI LA MBEYA WAKIWA WAMEUBEBA MWILI WA MC MWENZAO BARAKA CHAWE
ASKOFU WA  K.K.K.T  JOB MBWILO AKIONGOZA IBADA YA MAZISHI YA MC BARAKA CHAWE HUKO KIJIJINI KWAO ISYONJE
BAADHI YA NDUGU NA JAMAA WAKIMSIKILIZA ASKOFU WAKATI WAIBADA YA MAZISHI YA BARAKA CHAWE
WAKAZI WAMAENEO MBALI MBALI YA JIJI LA MBEYA NA VITONGOJI VYAKE WALIHUDHURIA MAZISHI YA MPENDWA WAO BARAKA CHAWE
MWILI WA MAREHEMU BARAKA CHAWE UKISHUSHWA KABURINI
ULITOKA MAVUMBINI UTARUDI TENA MAVUMBINI BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE AMEN
BABA NA MAMA WA MC BARAKA CHAWE WAKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI  LA MTOTO WAO
MTOTO WA PEKEE WA  MAREHEMU BARAKA CHAWE  RACHEL AKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA BABA YAKE
KWAKWELI WENGI WALIJITOKEZA KATIKA MAZISHI HAYO KIJIJINI ISYONJE LICHA YA KUWA NA MVUA ILIYOKUWA INAENDELEA KUNYESHA

PICHA NA MBEYA YETU 

MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KISHA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE MAJENGO JIJINI MBEYA

MTOTO ANETH AKIWA AMEOKOLEWA NA WASAMARIA WEMA HUKO MAJENGO

HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO

HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA  BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH


HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA HUYO MALAIKA WA MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA LAKINI KWA KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU CHOCHOTE

MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI

WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI


MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI

Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu  Habiba Mwakitabu amesema   kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.
Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo  alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo  anza kumpiga  .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .
Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.
Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.
Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.
PICHA KWA HISANI YA KALULUNGA
HABARI KWA HISANI YA EMANUEL MADAFA
 

No comments: