Sunday, November 4, 2012

Watu na matukio

TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA - MBEYA CENTRE, NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO YA SHAHADA YA UALIMU 2012/2013 

 Picha na matukio ni kwa hisani ya Kalulungablogspot.com 


MKUU WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI UNIVERSITY  MAKUMIRA,ANAWATANGAZIA WATANZANIA WOTE KUFUNGULIWA RASMI KWA TAWI JIPYA CHA CHUO HICHO UYOLE JIJINI MBEYA, AMBACHO AWALI KILIJULIKANA KAMA CHUO CHA UALIMU CHA KILUTHERI MBEYA.

HIVYO MKUU WA CHUO CHA TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA MBEYA CENTRE, ANAWATANGAZIA NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO YA SHAHADA YA UALIMU AMBAYO NI BACHELOR OF EDUCATION AND BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013.

CHUO KIPO KATIKA MAZINGIRA MAZURI YA KUSOMEA, MAKTABA YA KISASA, MTANDAO WA INTERNET NA WALIMU  WENYE UZOEFU,  HUDUMA YA AFYA INATOLEWA KATIKA ZAHANATI YA CHUO HICHO YENYE VIFAA VYA KISASA NA INATOA MATIBABU KWA  WANAFUNZI PAMOJA NA JAMII INAYOWAZUNGUKA,  PIA WALE AMBAO NI  WANACHAMA  WA MFUKO WA BIMA YA AFYA YA TAIFA (NHIF) WATAPATA HUDUMA  HIYO.

TUNAWAKARIBISHA WOTE KUJIUNGA NA WALE WANAOPENDA  KUHAMIA KATIKA CHUO, WAFIKE KATIKA OFISI ZETU ZILIZOPO UYOLE ENEO LA NSALAGA BARABARA KUU  IENDAYO DAR ES SALAAM  KARIBU NA KITUO CHA MAFUTA CHA LAKE OIL ILI WAWEZE KUJISAJILI NA KUPATA MAELEZO ZAIDI AU WATUME MAOMBI PAMOJA NA VYETI VYAO KWENYE BARUA PEPE IFUATAYO:-tumashuco2012@gmail.com.

MASOMO YATAANZA RASMI TAREHE 27/10/2012.UDAHILI UNAFANYIKA SASA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU ZIFUATAZO:-
0753 817 274, 0754 206 860, 0655 858 527

TAFADHALI UKISIKIA AU KUONA TANGAZO HILI MTAARIFU NA MWENZIO.
Bridgit Alfred atwaa taji la Redd's Miss Tanzania

Redd's Miss Tanzania 2012,Bridgit Alfred (katikati) akiwa na mshindi wa Pili,Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu,Edda Sylvester (kulia) mara baada ya kutangazwa mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2012 iliyomalizika katika ukumbi wa hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar.
 Redd's Miss Tanzania 2012,Bridgit Alfred akirurahia mara baada ta kutangazwa mshindi katika shindano lililomalizika hivi punge kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar

 Washereheshaji katika Onyesho la kumsaka Mlimbwende wa Redd's Miss Tanzania 2012 ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Taji Liundi na Kulia ni Jokate Mwegelo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakionyesha show yao mbele ya Watanzania katika Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
 Warembo wakipita katika jukwaani na Mavazi ya Ubunifu.
 Burudani ya Ngoma za Asili kutoka kwa Kundi la Wanne Star.
 Wadau wa Miss Tanzania wakibadilishana Mawazo.
 Wanahabari kazini.
Wadau kibao ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam
 Watu kibao ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
     Wanalibeneke mzigoni kama kawaida  

No comments: