Saturday, November 3, 2012

Matukio- Mbeya

LIVE !! MAHAFARI YA TANO YA CHUO KIKUU CHA TEKU MBEYA, WAHITIMU WAKIWA KATIKA MAANDAMANO KUELEKEA CHUO.

 BENDI IKIWA INAWASINDIKIZA HAHITIMU 
 KILA MTU ANA FURAHA SASA KAMA WANAVYO ONEKANA 
 MEDIA NAO HAWAPO NYUMA KUCHUKUA MATUKIO YA MOJA KWA MOJA 
 WOTE WAKIWA WENYE NYUSO ZA FURAHA MUDA HUU 
 WAHITIMU MBALIMBALI WAKIWA WANAELEKEA CHUONI SASA 
  MDAU MKUBWA WA MBEYA YETU, FRANK PESS AKIWA NA  JOHO LAKE KUELEKEA KATIKA MAHAFARI 
HAPA MAANDAMANO YANAENDELEA 

BREAKING NEWSSS WATOTO WAWILI WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI IMEZU INYALA MBEYA WAGONGWA NA ROLI NA KUFARIKI PAPO HAPO

Miili  ya wanafunzi wa shule ya msingi imezu ikichukuliwa na wanausalama watoto hao walikuwa wakivuka barabara akielekea shuleni ndipo roli hilo lilipowagonga na kukimbia huku miili ya watoto hao ikiwa imetawanyika vipandevipande ajali hiyo imetokea mida ya saa moja na nusu asubuhi
Watoto hao wamegongwa katika barabara kuu itokayo Zambia kwenda dsm maeneo ya imezu inyara wilaya ya mbeya vijijini
Waanchi kwa hasira wameamua kufunga barabara hiyo wakimtaka mkuu wa mkoa mbeya aje afike eneo la tukio  wamweleze kero zao za barabara hiyo kwani sasa inawamaliza wanakijiji hao kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo
Vijana wameshaanza kuweka mawe barabarani kuzuia magari yasipite na ukizingatia hii ndiyo barabara kuu ya magari yaendayo Malawi na zambia na mikoa ya jirani


Habari kamili tutawaletea baadae mpaka tunaondoka eneo la tukio mkuu wa mkoa Mbeya bado hajafika eneo la tukio 
na habari zisizo rasmi dereva aliyewagonga watoto hao kajisalimisha katika kituo cha polisi inyala

SAKATA LA MGOGORO WA MPAKA NDANI YA ZIWA NYASA KATI YA TANZANIA NA MALAWI LACHUKUA SURA MPYA. -Wazee Kyela watoboa siri nzito.



WAKATI nchi ya Malawi ikiendelea kushikilia msimamo wake, kuwa halali ya mpaka Mashariki mwa ziwa Nyasa kati yake na Tanzania unatenganishwa na ardhi ya Tanzania, Wazee wilayani Kyela, wametoboa siri na kuweka hadharani ukweli wake.
Wazee wengi waliotoa ushahidi juu ya ukweli wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi ndani ya ziwa nyasa, mbele ya msafara wa ziara ya siku moja ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe ni wale waishio kando kando ya ziwa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mstaafu, John Mwakipesile (70), ambaye katika maelezo yake akiwa wa kwanza, alisema anashangazwa na madai hayo mapya ya Malawi kuwa Ziwa lote ni miliki yao.
Alisema kitendo hicho cha nchi hiyo kukurupuka kinapaswa kuupuzwa kwa kuwa jambo hilo halina ukweli na linapingana na historia na desturi za kweli za maisha ya kawaida ya wananchi wa mpakani wa mataifa haya toka enzi za ukoloni.
Alisema madai ya Malawi hayajazingatia historia ya kweli ya ziwa hilo kwani madai yao yote ni kujaribu kuficha ukweli kwa kuwa yeye kama kizazi cha tatu hata siku moja hakuwahi kusikia kuwa ziwa lote ni mali ya nchi hiyo.
Alisema kuna ushahidi wa kutosha juu ya Tanzania kuwa miongoni mwa wamiliki wa ziwa hilo, kwani kuna mali za watanzania ikiwemo Makaburi yamepotelea ndani ya ziwa hilo baada ya kumezwa.
Alitolea mfano shule ya Msingi aliyesoma katika mwaka 1945 kuwa ilishamezwa na ziwa hilo, yakiwemo majengo ya baraza (Mahakama) katika kijiji alichozaliwa cha Mwaya katika wilayani humo.
“Mimi kwa umri wangu wa miaka 70 ni kizazi cha tatu katika Wilaya hii nakumbuka shule niliyosoma mwaka 1945 pale Mwaya nilipozaliwa ilishamezwa na Ziwa na ni umbali wa kilomita mbili toka pwani ya sasa kijijini hapo” alifafanua Mwakipesile.
Naye Maini Mwakisambwe(83), Mkazi wa kata ya Katumba songwe, alisema tangu azaliwa alikuwa akijua mpaka ni Mto Songwe ambao unaingiza maji ndani ya ziwa hilo na ndio uliotumika kama mpaka wa kuligawa ziwa klwa mataifa haya mawili.
Mbali na hilo, lakini pia wakiwa vijana walishuhudia viongozi wa serikali zote mbili wakiheshimu mpaka huo ndani ya ziwa , kwa kuwa hata waliposafiri toka upande mmoja kwenda mwingine kila wakifika eneo la Mto Songwe bendera ya uapane mmoja ilishushwa na kupandishwa ya upande mwingine.
Philipo Mwandemele(73) kabla ya kuanza kutoa maelezo yake alitoa kitabu kimoja kinachozungumzia maisha na desturi za wakazi wan chi hizi mbili kama nyaraka muhimu inayoweza kutumika kueleza ukweli juu ya sakata hilo la mpaka.
Katika kitabu hicho kilichoandikwa na mmishenari kutoka nchini Ujerumani Teodoro Mayers , anayedaiwa kufika wilayani humo kwa lengo la kueneza dini , katika ukurasa wake wa 31 kinathibitisha kuwa mwaka 1891 kulikuwa na mapatano kati ya Ujeruman na Uingereza kuwa mpaka wa Tanzania na Malawi ndani ya ziwa unaanzia pale Mto Songwe unamwaga maji ndani ya ziwa hilo.
Kutokana umuhimu wa kitabu hicho chenye jina la Wakonde, mila na Desturi za Wanyakyusa, Waziri wa Mambo ya Nje Membe alimuomba kuiazima serikali kwa muda ili kikarudufiwe na baadae kurejeshewa kwa lengo la kupata ushahidi sahihi.
Waziri Membe akihitimisha ziara hiyo alisema licha ya nchi ya Malawi kuonekana kusuasua katika vikao, kamwe Tanzania haitarudi nyuma kushughulikia mgogoro huo na kwamba hadi kufikia mwaka 2015 suala hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
Aliongeza kuwa maelezo na ushahidi huo uliokusanywa kwa wakazi wa wilaya ya Kyela utatumiwa na serikali katika Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi ya (ICJ), kama suluhu ya mashauriano ya pande mbili yatashindikana.
Katika mazungumzo juu ya mgogoro wa mpaka katika ziwa Nyasa yaliyofanyika Agosti mwaka huu nchini Malawi, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa wan chi hiyo Epraim Chiume, akihitimisha maelezo yake alisisitiza kuwa licha mgogoro huo kuhitaji busara zaidi , serikali yake inaamini kuwa mpaka kati ya nchi hizo upande wa mashariki mwa ziwa Nyasa unatenganishwa na ardhi ya Tanzania.

Kwahisani ya Moshi Mathias,Kyela.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 01/11/2012.





MNAMO TAREHE 31.10.2012 MAJIRA YA SAA 18:45HRS HUKO ENEO LA SAE MBILINYI JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.545 AZE SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA ABOOD ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA MUSSA S/O KILASI, MKAZI WA DAR ES SALAAM ILIGONGANA NA GARI T.610 ATQ/T253 APL SCANIA LORY ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA NA KUSABABISHA KIFO CHA CHARLES S/O KITELEKE, MIAKA 42, KONDAKTA WA BUS LA ABOOD MKAZI WA MOROGORO WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. 
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 23 WALIJERUHIWA KATI YAO 15 WALIPATA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA MAJERUHI 8 WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KATI YAO WANAUME NI 5 NA WANAWAKE NI 3 NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI. 
MAJERUHI WALIOLAZWA NI 1. NICUS S/O KAYUNI, MFIPA, 45, MFANYABIASHARA WA TUNDUMA 2. ANDREAS S/O MBILA, MKINGA, 32YRS, MFANYABIASHARA WA TUNDUMA 3. ZAMOYONI S/O WATSON, 28YRS, MSAFWA, MFANYABIASHARA WA TUNDUMA 4. VUMILIA S/O MWAZEMBE, MNYIHA, 31YRS, MKAZI WA MPEMBA 5. ALINAMAKA S/O MAHENGE 6. ANKA D/O MYAMBO, 45YRS, MZAMBIA 7. HILDA D/O CHILWA, 40 YRS, MKAZI WA ZAMBIA 8. GIFT D/O NANKALA, 40YRS, MKAZI WA MAMBWE ZAMBIA. 
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.610 ATQ/T.253 APL SCANIA AMBALO LILIKUWA LINAJARIBU KUPITA GARI JINGINE NA KWENDA KUGONGANA NA BASI HILO.
MADEREVA WA MAGARI YOTE MAWILI WAMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA MAGARI HAYO BADO YAPO ENEO LA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI NA VYOMBO VYA USAFIRI NA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIKO MADEREVA HAO AZITOE KWA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.


Signed By,
[  DIWANI  ATHUMANI – ACP  ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
TUKIO KAMILI: BASI LA ABOOD NAMBA T 545 AZE LA KUTOKEA DAR KWENDA TUNDUMA LAPATA AJALI MAENEO YA SAE(MBILINYI) BAADA YA KUGONGANA NA KENTA LILILO SABABISHA AJALI HIYO, MMOJA AFARIKI HAPO HAPO!

 Hivi ndivyo basi La Abood lilivyo pata ajali baada ya kugongana na Kenta
 Basi la Abood 
 Hivi ndivyo Basi Lilivyo Haribika 
 Haya ni mambaki ya Vioo vilivyo vunjika
 Baadhi ya vitu vikiwa vimemwagika chini
 Hili ni Scania ambalo lilikuwa likitokea Zambia 
 Dirisha likiwa limevunjika 
Baadhi ya Abiria wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa polisi 
Hapa ndipo basi la Abbod lilipo gonga 

*********************
BASI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU  KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.

KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA AMBAYE  ANAITWA CHALE KITELEKE AMBAYE PIA ALIKUWA NDIYE KONDA WA BASI HILO AMEFARIKI PAPO HAPO, PAMOJA NA MAJERUHI NANE AMBAO WAMEKIMBIZWA HOSPITALINI .

MPAKA TONE MEDIA LIVE GROUP AMBAO NI WAMILIKI WA MTANDAO HUU TUNATOKA ENEO LATUKIO HIZO NDIZO TAARIFA TUMEFANIKIWA KUZIPATA.

HABARI KAMILI ITAWAJIA KESHO BAADA YA KUPATA TAARIFA KUTOKA POLISI.

BREAKING NUUUZ JUST NOW: BASI LA ABOOD LAPATA AJALI ILIYO TOKANA NA KUGONGANA NA KENTA !

HABARI ZA UHAKIKA ZILIZO TUFIKIA KATIKA MEZA YETU YA HABARI ZINASEMA KWAMBA BASI LA ABOOD LIMEPATA AJALI MBAYA BAADA YA KUGONGANA NA KENTA MAENEO YA SAE JIJINI MBEYA. TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA KUTOKANA NA AJALI HIYO BAADHI YA ABILIA WAMEBANWA VIBAYA NA BASI HILO, PIA MPAKA SASA MVUA KUBWA INAENDELEA KUNYESHA, TONE MEDIA LIVE GROUP WAPO NJIANI KUELEKEA KATIKA TUKIO.

ENDELEA KUFUATILIA HAPA MBEYA YETU KWA TAARIFA ZAIDI
LIVE!! SAKATA LA UKOSEFU WA MAFUTA JIJINI MBEYA.. HALI NI TETE .. DALA DALA NI 1000 KITUO HADI KITUO

 Foleni ya kutosha kuelekea kufuata mafuta
 Boda nazo zinangoja mafuta hapa 
 Magari yakiwa  yameongozana foleni kwa ajili ya kutaka mafuta
 Barabara nyeupe watu wamepaki magari Majumbani kahuna mafuta 
 Daladala nazo shida , hizi ni baadhi ukipanda tuu kila kituo utalipia 1000

 Hii Gari ya kwanza mwisho ni ya Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu nae yupo kwa foleni 
MEMBE: HAKUNA MTU KUSEMA ZIWA LOTE NI LAKE.


WAZIRI MEMBE AKIWA KATUMBASONGWE.
Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiongea na wazee waishio Katumbasongwe, kando ya Ziwa Nyasa ndani ya Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.
Wakazi wa Katumbasongwe walimiminika kwa wingi kumsikiliza Mhe. Membe.
Wazee wa Katumbasongwe wakinyoosha mikono kujitambulisha umri wao wakati wa Mkutano wao na Waziri Membe uliofanyika jana Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.  Waziri Membe alikuwa Mkoani humo kwa ziara ya siku mbili ambapo alitembelea maeneo na makazi ya wananchi waishio ufukweni mwa Ziwa Nyasa.
WAZIRI MEMBE AKIWA MATEMA
Waziri Membe akiongea na wakazi wa Matema, Wilayani Kyela ambapo aliwasihi waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo.  Aidha, Mhe. Membe alisema Serikali inajitahidi kadri iwezavyo kutafuta suluhisho la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi. 
Wakazi wa Matema, waishio katika ufukwe wa Ziwa Nyasa, Wilayani Kyela wakimsikiliza Waziri Membe alipowatembelea jana.
Waziri Membe (hayupo pichani) pia alipata fursa ya kuongea na wazee wa Matema ikiwa ni sehemu ya mwisho wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Mbeya.  Katika mazungumzo yake na wazee hao, Waziri Membe aliwaeleza kuwa ziara hii ni sehemu ya kukusanya ushahidi muhimu kutokana na maelezo ya historia watakazochangia hususan tangu enzi ya ukoloni kuhusu Ziwa Nyasa.
Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO,Mbeya
“Hakuna mtu kusema Ziwa lote ni lake,” alisema Waziri Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kuongeza kuwa lazima kuwe na dhamana inayoonesha mipaka, kanuni na sheria ili kuondoa wingu la shaka yoyote hususan kwa Taifa lolote na wananchi wake.
Aidha, Waziri Membe aliongeza kuwa Serikali ina jukumu la kumaliza mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati yake na Malawi, na jitihada muhimu zinafanyika ili kuumaliza kwa amani na utulivu.
Waziri Membe aliyasema hayo jana mjini Mbeya alipokuwa akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, ambayo hiko chini ya Uenyekiti wa Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Akiainisha jitihada hizo, Mhe. Membe alisema kuwa Kamati ya Taifa inayojumuisha timu ya wanasheria na wataalamu wa mipaka imeundwa kwa madhumuni ya kutatua mgogoro huo na timu ya Malawi.  Pia kuna timu ya Kikosi Kazi chini ya Waziri Membe, ambayo jukumu lake ni kukusanya nyaraka na kumbukumbu muhimu za mgogoro huo tangu miaka ya 1890 hadi leo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri, baada ya Kikosi Kazi kumaliza kazi yake, kitawasilisha rasmi nyaraka kwa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua muhimu za Serikali zifanyiwe kazi.
Aidha, Mhe. Waziri alisema kuwa kuna umuhimu wa kutumia vyombo vingine ili kusaidia kutatua tatizo hili kama vile Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Baraza la Uongozi wa Wakuu wa Afrika la SADC (Leadership Forum – SADC), Umoja wa Afrika (AU) na ikiwezekana kuipeleka kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Kwa upande wake, Mhe. Kandoro alisema kuwa hali Mkoani Mbeya ni tulivu na kwamba maisha yanaendelea vizuri.  Alikanusha kuhusu taarifa zisizo za kweli zilizotangazwa kwenye mitandao kwamba mabomu yamerushwa Mkoani Mbeya hususan kwenye maeneo ya mpaka wa Ziwa Nyasa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa aligusia ukamatwaji wa wavuvi na mitumbwi kutoka Malawi ambayo ilikuja ufukweni mwa Tanzania, na kusisitiza kuwa hatua muhimu zilichukuliwa kwa kuzingatia na kuheshimu ujirani mwema. 
Katika ziara yake, Waziri Membe pia alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Bibi Margareth Malenga, ambapo alipata taarifa kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika mipaka ya Ziwa Nyasa, pamoja na mahusiano kati ya Wilaya ya Kyela na Wilaya ya Karonga nchini Malawi. Wilaya ya Kyela iko mpakani mwa Wilaya ya Karonga nchini Malawi.
Akisoma taarifa ya Wilaya yake, Bibi Malenga alisema “hali ya mipaka ni tulivu na kueleza kuwa hivi karibuni, mnamo tarehe 11 Oktoba, 2012 walipata ugeni wa Mhe. Mganda Chiume, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi na ujumbe wake akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Karonga nchini humo.” 
Kwa mujibu wa Bibi Malenga, lengo la ziara ya Waziri Chiume lilikuwa ni kukagua mpaka wa Ziwa Nyasa kwa upande wao lakini waliona ni vizuri waje Wilayani Kyela kuona hali ya mahusiano ilivyo baina ya wananchi wa upande wa Kyela na wale wa Karonga.  
Akiendelea na ziara yake, Waziri Membe pia alipata fursa ya kuongea na wazee alipotembelea maeneo ya Katumbasongwe na Matema yaliyopo katika ufukwe wa Ziwa Nyasa.
“Tumekuja hapa kupata ushahidi wenu wa kihistoria tangu enzi ya ukoloni ambao utazisaidia Kamati zilizoteuliwa kutatua mgogoro huu ili ziweze kukusanya kumbukumbu na kufanya kazi ipasavyo,” alisema Waziri Membe.
Aidha, Waziri Membe aliwahakikishia amani na utulivu wananchi wa Kyela, na kusema kuwa “Serikali inajitahidi kadri iwezavyo kutatua mgogoro huu kwa njia ya kidiplomasia na hata kama ikiwezekana kwenda ICJ.”
Aidha, Mhe. Membe kabla ya kumaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Mbeya jana, pia alitembelea mipaka ya Kasumulu Katumbasongwe na Matema kwenye ufukwe wa Ziwa Nyasa, katika Wilaya ya Kyela ambapo alizungumza kwa kina na 
Picha na maelezo,  ni kutoka kwa Jose Mwaisango wa Mbeya Yetu Blogspot .
Abarikiwe sana kwa kazi zake!

No comments: